Our Clubs.

...

Sunday, March 5, 2017

UPINDE NA HISTORIA YAKE KATIKA WUSHU,KUANZIA MWAKA 1977 HADI 2017.


HII  NI HISTORIA YANGU  KATIKA  WUSHU KUTOKA NILIKOTOKEA HADI HAPA

NILIPO LEO TAREHE 06/03/2017



Ninaitwa Sultani Kassim Upinde Ngwaya Ngapoleka mzaliwa wa MkambaWilaya Ya Mkuranga Tarafa Ya Mkamba Kata Ya Kisegese Kijiji cha VianziKitongoji Changedele.Nilizaliwa tarehe 20/08/1956.Nimeanza 

kuhamasika na kupenda kujifunza sanaa zamapigano kupitia kwa rafiki yangu aitwae Jumanne Ngwele Mwaka 1977Mtoni  Kwa Azizi Aliy Mtaa Wa Bostani.


Masta jumanne ngwele alikuwa anajifunza Gujuluu katika shule ya Zanakikwa Sensei Magoma wakati huo. Nami nikahamasika hatimaye akaanzakunifunza.


Lakini haikuchukua muda Jumanne alifariki, Kutoka hapo sikupatamwalimu wakunifundisha.Ilipofika mwaka 2000 nilihamia mbagara charambe mtaa wa mianzini, hapahamasa na mapenzi ya hii sanaa yaliibuka tena 

nilipokutana na MuharamiShaweji Mitete, Nilimkuta katika Gofu La Kantini  ya Tanita. Wakati huo, nilimkuta na wenzake kumi, Misilu, Luka, Mrisho, Abdala, Msiba, Kamanda Katambo, Kihiyo,Kazi Mnyunguna wengine.Nilio, wakuta 

wakifanya mazoezi Mitete  akiwa mwalimu  anafundisha staili iliyokuwa anaiita Kota Gushu.

Nikaomba utartibu wa kujiunga hatimae nikajiunga mimi na watoto wangu sita.

Nao ni:-Kassim  S. UpindeIbrahimu  S. UpindeYusuph  S. UpindeOmari   S. UpindeSaidi  S. UpindeSophia  S. UpindeKutoka hapo Tempo likaanza kushamili watu wakawa wanajiunga kwa wingi.

Bwana Muharami mitete akawa ana waleta walimu wa staili hii yamapigano wanaocheza michezo tofauti tofauti ili kuongeza nguvu yaufundishaji.Alimleta masta Cholo ambaye alifundisha  kombati kilaAlimleta Hamisi Mchina  mchezowake nimeusahau jina.


Alimleta Baba Rama  maarufu  kwajina la (FUU) wengine walimwuitaGujuluu huyu alifundisha shaolin kung – fu


Tempo lilipozidi kushamili Baba Rama alimualika   Mzee Saidi Kibe kujakuona  maendeleo ya vijana.Alivyokuja Mzee Kibe na kuona hali hiyo nae alimualika Mzee Taiga naowakati huo ndio walikua  wadau wakapendekeza Clabu hii iitwe TAI CLUB.


Club iliendelea kujulikana Mbagala nzima, tukaanza kupata changamotoza ndugu zetu wa Shotokan Karate wakidai tunachokicheza  hakitusaidiihapa Nchini. Hakuna Shaolin Kung - fu  tunaongopeana tu ni boratubadili staili tucheze karate watatuletea mwalimu wa Shotokani.



Tukalazimika kuanza  kuitangaza kupitia matamasha na kutembelea vilabumbalimbali vya Karate na vya Shaolin. Mpaka  Kung – fu  ikaanzakutambulika Wilaya ya Temeke.


Ilipofika mwaka 2006 Mzee Kibe  na Mzee Taiga waliamua kutukabidhisatefiketi ya  Msasani Tai Club.
Tulipotaka kufanya taratibu za uhamisho Afisa Utamaduni  wa Kinondoniwa wakati huo alikuwa Mr. Chaurembo , 

alitushauri tusiihamishe balitusajili ya kwetu.Ndipo ilipofika tarehe 05/07/2006 tukaisajili mbagara  Tai ShaolinKung – fu . Toka kuanza Dunia hapa Tanzania  haijawahi  kusajiliwaClubu yoyote kwajina la Shaolin Kung – fu hii ndiyo ya kwanza.


Tukazalisha walimu kadhaa wa Kung – fu kisha tukaanza kuwasambaza mikoaniIlipofika tarehe 08/06/2009 Tanzania tulipokea ugeni wa timu ya Wushutoka China. Walifanya shoo yaokibaha Firbert Bayi Sekondary School


Mbagara Tai  Club  tulishiriki  pamoja  katika shoohizo pamoja na ya chuo kikuu Dar es salaam pia tulishiriki.Kitendo hiki cha kushiriki shoo mbili hizi kilipelekea   makamo waRais wa Chinese Wushu  ndiye aliyekuwa kiongozi wa msafara huo.Aliiomba serikali ya China na ya Tanzania zisimamie uudwaji wa Chamacha Wushu Tanzania.Mpaka januari 2010 tayari chama cha Wushu Tanzania kilikuwa kimeshasajiliwa kwa jina la Tanzania Wushu Association (T.W.A)  chini ya uongozi waSULTANI UPINDE NA MUHARAMI S. MITETE.


Toka hapo tukawania kazi ya kubadilisha matawi ya Tai Club yote nakusimamia usajilin wa vilabu vya mikoani na kuhamasisha wadau
waliokuwa wanacheza Kung – fu  vichochoroni kujitokeza , tukasimamiausajiri wa vilabu vyao hatimae kuwasajili katika chama cha Wushu kazi
hii yote tuliifanya watu wawili mimi na Mitete tukisaidiwa na HarufaniMadhurui (Mr Mazu).    Muharami akiwa kama Raisi wa T.W.A, Mazu Makamo waRaisi, Fredi Maiga katibu Mkuu na Mimi nikiwa katibu Msaidizi,
Mbokigwe Bwana Mipango. Wa Maingu Hazina , Omari Maisa  HazinaMsaidizi .
Tuliyo wahi kuyafanya katika uongozi huu:-


Kumsafirisha  Mitete kwenda Beijing kujiunga IWUF,
Kuwasafirisha vijana wawili (2) kwenda China kujifunza  sarakasi vijana hao niOmari UpindeRamadhani Maneno Issa Cobra.tulipeleka vijana wa 2 katika mafunzo nchini China,
Muharami
Cobra,
Muhina,
Ayubu,
Tulipeleka vijana wanane Nchini uturuki katka mashindano ya watotoDuniani wenye umri chini ya miaka 18 Tanzania tulishika nafasi yakwanza Afrika na ya nane (8) Duniani





Tulipeleka vinaja wawili (2) Libiya katika mashindano ya Afrika nao niAbdala MuhinaUswege MwasebaTulishika  nafasi ya tatu (3)
Tulipeleka vijana wawili China kupata mafunzo nao ni:-R. MshanaZ. zola toka tarime,
Tuliwapeleka vijana watatu malawi kushiriki mafunzo ya mchezo wa Zurhani nao niAbdala NyoniAmani Rashidi (Zinja)Juma Mdadila,


Tuliandaa mashindano ya kwanza ya wushu hapa Nchini Tanzania 2011yalifanyika Coco Beach.
Kusimamia uchaguzi wa vilabu vyote vya wushu hapa Nchini,
Tulipeleka vijana wanne China kwenye mafunzo nao ni
Maulidi NgusilaSaidi MfaumeUswege MasebaYusuph Upinde
Nimesimamia  kusajiliwa  kwa timu ambazo naziita ni Famili nazo ni:-


1. Ngapoleka Wushu Club
2. Dragoni Wushu Club
3. Changamkeni  Wushu Club timu hii ipo katika sekondari ya mikwambe
wilaya ya  kigamboni inayoitwa changanyikeni,
4. ngwaya shaolin Kung – fu  na pia nimesimamia ujengwaji wa kituo cha kung – fu kikubwakilichopo kisiwani Mafia  nikishirikiana naDokta Bobu, ambacho tunatarajia kukizindua mwezi wa  6 2017
kwa ujumla hii ndio histori yangu kwa ufupi ndani ya wushu.Mpaka hii leo tarehe 06/03/2017,

,bado naendelea nikiwa katibu msaidiziwa T.W.A Taifa.



AHSANTENI KWA KUISOMA HISTORIA YANGU NDANI YA WUSHU.







KWA YOYOTE ANAETAKA KUTOA HISTORIA YAKE, AU CHOCHOTE, KUHUSU SANAA ZA MAPIGANO(martial arts) YA AINA YYOYOTE 
KUNG FU, KARATE, BOXING,
NK
WASILIANA NAMI KWA
0655326142 / 0785681680
au
NIANDIKIE KUPITIA
mfaumetz@gmail.com

No comments:

Post a Comment